Tanica yazindua Duka na Mgahawa Mpya na wa kwanza wa kahawa ya Tanica

Tanica yazindua Duka na Mgahawa Mpya na wa kwanza wa kahawa ya Tanica

Tanica yazindua mgahawa mpya na wa kwanza kabisa katika historia ya Tanica siku ya Jumamosi tarehe 12/09/2020 katika eneo La TRS Fitness and Club (Zamani ikijulikana kama KIIZA Health Club) mkabala na Hotel ya Victorious perch, ikiwa ni juhudi za dhati za Kujitangaza na kukuza masoko ya kahawa ndani na nje ya Nchi ya Tanzania. Pamoja na Mgahawa huo, Tanica Imezindua Kifungasha kipya cha kahawa ya Kukaanga na Kusaga (Roasted and Ground Coffee), Website mpya na ya Kisasa pamoja na Kumtangaza msambazaji mkuu wa kahawa ya Tanica Katika Mkoa wa Kagera ndugu Philbert Rukiko Maarufu kama Mzee Kitwe.

Akizundua mgahawa huo, Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mheshimiwa Brigedia Generali Marco Gaguti amesema, ufunguzi wa mgahawa huo iwe ni chachu na changamoto ya kufungua mingine mingi zaidi ili kuweza kukuza zaidi masoko na kubadilisha Taswira nzima ya Utendaji wa Kiwanda cha Tanica. Mkuu wa mkoa amemshukuru na kumpongeza ndugu Philbert Rukiko (Kitwe Shop and Distributors) kwa kuwa tayari kufanya kazi kwa karibu na Tanica. Pia amepongeza sana juhudi zinazofanywa na Meneja wa Kiwanda ndugu Rodness Milton na timu nzima ya Tanica katika juhudi za kuiinua Tanica.

Katibu Tawala wa Mkoa wa kagera ndugu Profesa Faustine Kamuzora, ameongeza na Kusema kuwa Tanica inabidi iongeze ubunifu katika kutoa huduma za migahawa ya kahawa ili kuendana na soko la dunia la migahawa ya kahawa maarufu kama Coffee bar

Katika wasilisho alilolifanya Meneja wa Masoko Ndugu Franco Maulid aliainisha faida mbalimbali za kufungua migahawa hiyo ikiwa ni pamoja na kuleta chachu ya maendeleo na ubunifu katika utendaji na kuitangaza Tanica katika soko la ndani na nje ya nchi.

Huduma zitakazopatikana katika mgahawa huo ni Espresso, Capuccino, Café latte, Americano, Spice Latte, Moccha Latte na Machiato.

One thought on “Tanica yazindua Duka na Mgahawa Mpya na wa kwanza wa kahawa ya Tanica”

  1. NGABILE NYARIJOJO November 8, 2020 at 9:16 am

    Nawapongeza sanaa kwa hatua hiyo nzuri
    Lakini pia nichukue nafasi hii kuomba Kazi katika mgahawa huo

Add a Comment

Your email address will not be published.