Mkuu wa Mkoa awataka TANICA kufungua “Coffee Shop and Bar”

Mkuu wa mkoa wa Kagera Mheshimiwa Brigadier General Marco Gaguti amewataka Tanica kufungua mgahawa wa kahawa maarufu kama Coffee Shops ili kuweza kuitangaza Zaidi kahawa ya Tanica kwa wenyeji na wageni mbalimbali wanaofika katika mkoa wa Kagera. Ameyasema hayo akiwa katika banda la Tanica katika maadhimishio ya sikukuu ya wakulima NANE NANE 2020 yaliyofanyika viwanja vya Kyakailabwa Manispaa ya Bukoba Mjini.

Pamoja na hilo amewasisitiza wanakagera na watanzania kwa ujumla kutumia kahawa ya Tanica kutokana na faida zake mbalimbali kiafya ikiwemo kupunguza uwezekano wa kupata kisukari aina ya pili, Magonjwa ya Kibofu cha mkojo, Ugonjwa wa kusahau, Kupunguza uwezo wa kupata saratani ya ini, tezi dume na utumbo mpana, ugonjwa wa kutetemeka na Kupunguza msongo wa mawazo.

Add a Comment

Your email address will not be published.