Msimu wa Kahawa Kagera wafunguliwa rasmi

Msimu wa Kahawa Kagera wafunguliwa rasmi

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti azindua rasmi msimu wa Kahawa wa mwaka 2020/2021 ikiwa ni pamoja na kutangaza bei ya malipo ya awali shilingi 1200 kila kilo ya kahawa ya maganda kwa Vyama Vikuu vya Ushirika vya KCU 1990 Limited, KDCU Limited na Ngara Farmers.

Vyama vya KCU na KDCU vyahimizwa kusimamia kiwanda cha TANICA ili kifanya vizuri kwani vyama hivyo vinamiliki hisa za asilimia 87% kwenye kiwanda hicho. Hivyo ikifanya vizuri ni faida kwa vyama hivo na kwa mkulima wa chini pia.

Naye Mtendaji Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. Japhet Justine katika hafla hiyo ya ufunguzi wa msimu wa kahawa mwaka 2020/2021 alisema kuwa Vyama Vikuu vya Ushirika Mkoani Kagera vimekuwa viaminifu tangu mwaka 2018 benki ya TADB ilipoanza kuvipa mkopo ambapo msimu wa mwaka 2018 Benki hiyo ilitoa   bilioni 30 na zililipwa zote, msimu 2019 Benki ilitoa bilioni 23 na zote zililipwa.

Kuanzia Juni 9, 2020 wakulima wa zao la kahawa Mkoani Kagera wanahamasishwa kuanza kukusanya kahawa katika Vyama  vyao vya Msingi na fedha ya malipo ya awali ipo tayari kwaajili ya  kuwalipa.

Add a Comment

Your email address will not be published.