TANICA PLC inajivunia kutangaza kuwa imefanikiwa kuwa Mshindi wa Tatu katika kundi la Makampuni na Viwanda vilivyoshiriki maonesho ya Nanenane yaliyofanyika katika Viwanja vya Kyakailabwa, Manispaa ya Bukoba, Mkoani Kagera.
Tuzo hii ya Best Award imetolewa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mkoa wa Kagera, kutambua mchango na ushiriki wetu. Maonesho hayo yalifanyika kuanzia Tarehe 01 hadi 08 Agosti 2025.
Tunawashukuru wateja wetu, wadau, na wafanyakazi wote kwa mchango wao katika kufanikisha mafanikio haya.
Endelea kutembelea tovuti na mitandao yetu ya kijamii kwa habari zaidi na bidhaa bora zaidi kutoka kwetu.

